Jumapili 19 Oktoba 2025 - 00:17
Tabliigh bila mchango wa utafiti haiwezi kufanikiwa/ Tusisahau umuhimu wa mtazamo wa ijtihaadi

Hawza/ Mkurugenzi wa hawza, Ayatullah Alireza A‘rafi, amesisitiza kuwa kujitolea katika masuala ya utafiti ni sharti muhimu kwa mafanikio ya shughuli za kielimu na za tabligh (ulinganiaji), akibainisha kuwa jukumu kuu la wasaidizi wa utafiti ni kulea wataalamu wenye uwezo na kuzalisha fikra mpya.

Kwa mujibu wa mwandishi wa Shirika la Habari la Hawza, Ayatullah A‘rafi akizungumza katika siku ya pili ya mkutano wa 13 wa wasaidizi wa utafiti wa hawza za mikoa na maeneo maalumu uliofanyika katika ukumbi wa “Amin” katika kituo cha uongozi wa hawza, aliwashukuru waandaaji wa mkutano huo hususan Hujjatul-Islam wal-Muslimin Abbasii, msaidizi wa utafiti wa hawza.

Amesema kuwa kwa kuzingatia aya tukufu za Qur’ani, tunaona wazi jinsi mwanadamu alivyo na haja na umasikini wa asili mbele ya Mwenyezi Mungu, hivyo inatupasa kumwomba Yeye atuongoze katika njia ya uongofu na ustawi, na Atupe utajiri wa kiroho.

Fikra ya “ufukara wa kiasili” katika ulimwengu

Ayatullah A‘rafi alibainisha kuwa; ulimwengu mzima una ufukara wa asili ambao unatofautiana na aina nyingine za umasikini tunazozijua. Alisema: “Kitu cha msingi ni kufahamu kwamba asili ya uwepo wote inategemea ulimwengu mwingine, na katika dunia hii yenye kufa sisi tuko katika hali ya ufukara wa kina. Hata hivyo, ukamilifu uliopo ndani ya viumbe nao ni aina ya ufukara, kwani ni kupitia fadhila ya kwanza ya Mwenyezi Mungu ndipo ulimwengu unapata heshima na nafasi yake.”

Njia pekee ya kuondoa ufukara huu ni kumuabudi Mwenyezi Mungu

Akaongeza kuwa: “Dini imekuja ili kumkumbusha mwanadamu kuhusu uhusiano na utegemezi wake huu, na kwamba njia pekee ya kuondoa ufukara na kupata ufanisi ni kupitia kumuabudu Mwenyezi Mungu. Hivyo basi, ukamilifu wa mwanadamu ni katika kutambua ufukara huu.” Akarejea maneno ya Mtume (s.a.w.w): “الفقر فخري” – Umasikini (wa kiroho) ndio fahari yangu.

Ayatullah A‘rafi aliongeza kuwa; utambuzi wa ufukara huu una viwango mbalimbali; mtu akifika katika kiwango cha juu cha kuelewa na kuhisi hali hiyo kwa akili na moyo, basi anafikia daraja la shuhudi (utambuzi wa kipekee wa kiroho). “Kadiri upeo wa uwepo wa mtu unavyopanuka, ndivyo unyenyekevu wake mbele ya Mungu unavyoongezeka,”.

Mkurugenzi huyo wa hawza alifafanua kuwa; falsafa kuu ya kuwepo hawza ni katika mambo mawili makuu:

1. Kulea nguvu kazi yenye uwezo, ambapo elimu, utafiti, na malezi ya kiroho (tazkiya) lazima viunganishwe pamoja ili kutoa wanafunzi wenye uwezo wa kujibu mahitaji ya jamii.

2. Kuzalisha fikra na nadharia mpya, na kujishughulisha na kukuza mawazo sahihi na asili ya Kiislamu.

Alisema bila shaka, utafiti unachukua nafasi ya msingi katika masuala yote mawili, huku elimu ikiwa ndio nguzo kuu inayowezesha malezi ya wataalamu na uzalishaji wa fikra.

Hatua kubwa za hawza katika teknolojia na akili bandia

Ayatullah A‘rafi aliongeza kuwa, kwa neema ya Mwenyezi Mungu, hawza zimepiga hatua kubwa katika teknolojia za kisasa na akili bandia (AI), hususan katika ujenzi wa miundombinu yake, na kwamba taarifa zaidi kuhusu maendeleo hayo zitatolewa baadaye.

Alionesha pia kuwa mustakabali unaleta fursa kubwa ambazo lazima zitumiwe ipasavyo. Akasema: “Akili bandia inaleta changamoto na wakati huo huo fursa katika njia ya kueneza na kuzalisha maarifa ya Kiislamu na kibinadamu, hivyo hatupaswi kupuuza jambo hili.”

Umuhimu wa mtazamo wa ijtihadu kwenye tafiti za Kiislamu

Akihitimisha, alisema: “Tafiti tunazofanya katika nyanja za sayansi za kibinadamu na Kiislamu zina viwango tofauti, lakini katika sayansi za Kiislamu tunahitaji ijtihad na uelewa wa kina wa mafundisho ya dini, kwani masuala haya yanahusiana na dini na lazima yawe na hoja sahihi za kidini.

Hata kama si kila mtafiti ni mujitahidi, lakini hatupaswi kusahau umuhimu wa mtazamo wa ijtihadi, ili tuweze kunufaika na urithi mkubwa tulio nao.”

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha